1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brasilia.Lula da Silva ashinda tena uchaguzi nchini Brazil.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxi

Rais wa sasa wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ameshinda kipindi kingine cha Urais nchini humo.

Lula da Silva ameshinda kwa zaidi ya asilimia sitini ya kura na kumshinda mpinzani wake Geraldo Alckmin katika kile maofisa wanachokiita ni ushindi laini kabisa wa awamu ya pili.

Akisherehekea ushindi wake, Rais Lula ameahidi kujenga misingi imara na bora zaidi nchini Brazil.

Rais Luiz Inacio Lula da Silva ataapishwa tarehe mosi Januari mwakani.