BRASILIA:Brazil yaomboleza vifo vya ajali ya ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRASILIA:Brazil yaomboleza vifo vya ajali ya ndege

Rais Lula da Silva wa Brazil ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali ya ndege ambapo watu 155 wamekufa.

Habari zinasema hakuna alienusurika katika ajali ya ndege hiyo iliyoanguka katika misitu ya Amazon.

Askari waliopelekwa katika sehemu hiyo ya ajali walilazimika kufyeka misitu mikubwa ili kuziwezesha helikopta kutua.

Ndege hiyo ya abiria ilikuwa inatoka mji wa Manaus kaskazini mwa Brazil ikielekea mji mku Brasilia.

Kilichosababisha ajali ya ndege hiyo bado hakijajulikana lakini maafisa wa usafiri wa anga wanatuhumu kuwa iligongana na ndege nyingine ndogo iliyoweza kutua salama baada ya dafrao hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com