1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOSTON :waziri Mkuu wa Ufaransa aitaka Marekani iondoe majeshi y ake kutoka Irak

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHx

Waziri Mkuu wa Ufaransa bwana Dominique de Villepin ameitaka Marekani iondoe majeshi yake kutoka Irak hadi itakapofika mwaka kesho .

Waziri mkuu huyo ameeleza kuwa vita vya nchini Irak vimeharibu jina la Marekani.

Akizungumza kwenye chuo kikuu cha Havard karibu na Boston waziri mkuu huyo amezitaka Marekani na Ulaya zichukue hatua za pamoja katika kuheshimu haki za mataifa mengine na hasa katika mashariki ya kati.