1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn. Mgomo waendelea D.T.Kom.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2B

Sekta ya huduma katika chama cha wafanyakazi cha Ver.di kimepanua hatua yake ya mgomo katika shirika la simu nchini Ujerumani , Deutsche Telekom ambalo lilikuwa linahodhi huduma zote za simu.

Chama hicho cha wafanyakazi kimewataka kiasi cha wafanyakazi 14,000 wa Telekom nchini Ujerumani kutofanya kazi.

Mgomo huo unafanyika kupinga mipango ya kampuni hilo ya kufanya mageuzi.

Telekom inataka kuhamisha nafasi 50,000 za kazi kwenda katika huduma mpya za wateja zilizoundwa ambako wafanyakazi watafanyakazi kwa saa nyingi kwa malipo kidogo.