1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bishkek.Raia waandamana nchini Krygyzstan.

Maelfu ya waaandamanaji nchini Kyrgyzstan, waliandamana mbele ya ofisi ya Rais Kurmanbek Bakiyev iliyopo mji mkuu wa nchi hiyo Bishek.

Wakati huo huo Rais amemfukuza kazi waziri wa mambo ya ndani na kuahidi kumteuwa mtu ambae hatatumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Maandamano hayo yamekuja kufuatia Rais kushindwa kufika Bungeni kuwasilimsha mswaada wa mageuzi ya katiba.

Upande waUpinzani umesema mapendekezo hayo yanafanya mambo kuzidi kuwa mabaya.

Maandamano dhidi ya Rais Bakiyev yamekuwa yakiendelea kwa siku ya tano mfululizo, wapinzani wake wanamlaumu kwa kushindwa kupambana na umasikini na kuachilia mbali mageuzi ya kidemokrasi aliyoahidi katika kampeni za uchaguzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com