1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK: Waziri mkuu mpya aidhinishwa

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWi

Bunge nchini Kyrgystan limemkubali waziri mkuu mpya. Hatua hiyo inamaliza mgogoro wa majuma mawili baina ya wagombewa wawili waliong´ang´ania wadhifa huo. Azim Isabekov alitangazwa waziri mkuu alipopata ushidni bungeni wa kura 57 kwa 4.

Kiongozi huyo wa umri wa miaka 46, aliyekuwa zamani waziri wa kilimo, ni mwanasiasa mahiri na kiongozi wa zamani wa utumishi wa rais wa Kyrgistan, Kurmanbek Bakiyev.

Hapo awali, rais Bakiyev alimteua waziri mkuu wa zamani, Felix Kulov, aendelee na wadhifa wa waziri mkuu nchini humo. Lakini wabunge walikataa mara mbili uteuzi wa Kulov.