1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biashara ya silaha kati ya Ufaransa na Libya

3 Agosti 2007

Ufaransa imefunga mikataba gani majuzi na Libya ? hilo ni swali linaloulizwa na baadhi ya wabunge wa Ufaransa.

https://p.dw.com/p/CHA4

Wanasiasa wa Ufaransa, wanadaiwaelezwe ni biashara gani ya silaha imeafikiwa majuzi kati ya rais wa Ufaransa, Nocolas Sarkozy na Libya.

Ujerumani hasa ingependelea kuseleleza marufuku ya kuuziwa silaha Libya,lakini mwana wa Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi-Saif amekueleza kuachwa huru kwa Libya kununua upya silaha kutoka nchi za magharibi.

Mtoto wa Muamar Gadhafi Saif Al Islam,ameliambia gazeti la Ufaransa la “Le Monde” kinu cha kinuklia cha kugeuza maji ya chumvi ya baharini kuwa ya kunywa ambacho Ufaransa imeafikiana na Libya kuijengea si muhimu hivyo.

Kwani,Libya inaweza kutumia mafuta yake ya petroli kuendeshea kinu kama hicho.Muhimu ni kwamba nchi ya magharibi kwa mara ya kwanza imekiuka marufuku iliowekewa Libya ya kuuziwa silaha na nchi hizo.

Ufaransa, itaiuzia Libya makombora ya kupamnbana na vifaru yenye thamani ya Euro milioni 100.Isitoshe, Ufaransa itaunda kiwanda cha silaha nchini Libya.

Ujerumani hasa imejizuwia kuiuzia Libya silaha tangu 2004.Kubadili msimamo huo, mazungumzo juu ya kuachwa huru kwa wale wauuguzi wa kibulgaria waliohukumiwa adhabu ya kifo nchini Libya ilikua fursa nzuri kabisa.Je, hiyo ni sawa au si sawa ?

Rais Nocalas Zarkozy wa Ufaransa alizuru Libya wiki iliopita.Yeye akijibu swali iwapo Libya kwa kuridhia kuwaacha huru mahabusu wake iliahidiwa kitu alisema la.

Na waziri wake wa mambo ya nje Bernard Kouchner,hakuonesha angependa kuzungumza mengi:

“Hakujakuwapo ahadi ya kutoa jaza yoyote kwa Libya.”

Lakini hata katika kundi la wabunge wa chama cha rais Sarkozy UMP,kuna wanaoelemea zaidi kuamini asemayo motto wa Gadhafi kuliko rais wao.

Ila kali na wazi zimetoka kwa mbunge Claude Goasguen alietaka kujua ni mikataba gani Ufaransa imefunga na Libya:

“Rais wa Ufaransa amechaguliwa kutokana na ahadi zake alizotoa kukomesha tabia kama hii ya diplomasia ya sirisiri na yakuficha mambo.Waziri wake wa nje lazima aweze kuwaarifu wabunge ni mikataba gani imefungwa na Libya.”

Wabunge wa vyama vya kisoshalisti na kikoministi wamefika hata umbali wa kudai kuundwe halmashauri ya uchunguzi.Katika mabishano ya siasa za ndani nchini Ufaransa kuhusu Libya,inahusu pia staili ya uongozi ya rais Sarkozy.

Mchango gani anatoa mkewe rais Sarkozy-aitwae Cecilia ambae kabla ziara ya mumewe mjini Tripoli alitangulia huko na ahalfu akafuatana na wauguzi walioachwa huru hadi Bulgaria ?

Swali jengine:mawaziri wa Sarkozy wana madaraka gani ya kutenda chini yake ?

Kwani, imedhihirika katika kila uwanja,rais sarkozy anashika usukani.Sarkozy amewachagua wajumbe wengi wa upinzani wa chama cha Kisoshalist- katika serikali yake-miongoni mwao waziri wa nje Kouchner.