1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlusconi apinga mageuzi ya sheria za uchaguzi

31 Januari 2008
https://p.dw.com/p/D05d

Kiongozi wa upinzani nchini Italia, Silvio Berlusconi, amekataa pendekezo la kuubadili mfumo wa kupigia kura nchini humo lakini akasisitiza uchaguzi wa mapema ufanyike.

Rais wa Italia, Giorgio Napolitano, ambaye amekuwa akiongoza juhudi za kuutanzua mzozo wa kisiasa nchini humo, uliosabaishwa na kujiuzulu kwa waziri mkuu Romano Prodi wiki iliyopita, amemtaka spika wa bunge, Franco Marini, atafakari ikiwa serikali ya mpito itaweza kupitisha mabadiliko ya sheria za uchaguzi.

Wachambuzi wana wasiwasi ikiwa inawezekana kuubadili mfumo wa uchaguzi nchini Italia ikizingatiwa hali ya sasa ya kisiasa nchini humo.