BERLIN:waziri wa ulinzi wa Ujerumani kufanya ziara nchini Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:waziri wa ulinzi wa Ujerumani kufanya ziara nchini Israel

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Franz Joseph Jung anatarajiwa kuanza ziara nchini Israel ambapo atakutana na waziri mwanzake Amir Perez ili kujadili mkasa uliotokea hivi karibuni ambapo ndege za kivita za Israel ziliishtua manowari ya doria ya Ujerumani katika pwani ya Lebanon

Wizara ya ulinzi imesema kuwa hali ya kutoelewana ilitokea na kusababisha mkasa huo ambao haukuleta madhara yoyote.

Kwa mujibu wa habari ziizokaririwa na gazeti la Focus la hapa nchini, pamekuwapo na matukio ya hatari baina ya majeshi ya Israel na ya Ujerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com