1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Watuhumiwa watatu wafikikshwa mahakamani

6 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSE


Polisi nchini Ujerumani wanawasaka watuhumiwa kumi wanaodaiwa kuhusika na njama za mashambulio ya kigaidi dhidi ya vituo vya Marekani humu nchini.

Watuhumiwa watatu waliokamatwa jana wamefikishwa mbele ya mahakama kujibu mashtaka ya kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi baada ya upelelezi wa miezi kadhaa.

Watuhumiwa hao wawili raia wa Ujerumani na mwingine raia wa Uturuki inadaiwa walipanga kushambulia kwa mabomu kambi za jeshi la Marekani nchini humu, uwanja wa ndege wa Frankfurt, sehemu za disko, vilabu vya pombe vinavyotemebelewa zaidi na raia wa Marekani. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa na watu wanaowapa misaada ndani na nje ya Ujerumani.

Afisa wa cheo cha juu wa wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani amefahamisha kwamba watuhumiwa hao walipokea mafunzo nchini Pakistan kabla ya kuanzisha kikundi cha Islamic Jihad ambacho hakijulikani lakini ni kikundi kilicho na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema lengo lao lilikua kuangamiza idadi kubwa ya binadamu, bibi Merkel amewashukuru walinda usalama wa Ujerumani.