Berlin.Ujerumani yathibitisha kushambuliwa manuari yake na ndege za Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin.Ujerumani yathibitisha kushambuliwa manuari yake na ndege za Israel.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amethibitisha taarifa za gazeti kwamba ndege mbili za kijeshi za Israel zimehusika na hujuma za kijeshi dhidi ya manuari ya kijerumani inayopiga doria katika mwambao wa Lebanon.

Kulingana na toleo la leo la gazeti la Tagesspiegel, ndege mbili za kijeshi za Israel chapa F16, ziliifyatua risasi zilipopita juu ya manuari ya kijarumani inayotumikia juhudi za amani za Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.

Waziri wa ulinzi wa Israel Amir Perets amekanusha kwamba hakuna risasi zozote zilizofyatuliwa, lakini msemaji wa jeshi la Israel amesema, ndege mbili ziliizingira Helkopta ya Ujerumani ambayo wamedai hawakuitambua.

Waziri Peretz na Jung walizungumza na wamepanga kukutana nchini Israel wiki ijayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com