1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani yamimina misaada Somalia

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4t

Ujerumani itatoa msaada nyongeza wa euro millioni 1.5 kwa ajili ya kuipa msukumo miradi ya misada kwa binaadam nchini Somalia.

Kupitia Shirika linalosaidia maeneo ya majanga la DIAKONIE zitatolewa euro laki tano kwa ajili ya msaada wa chakula kwa maeneo ya nje na mji mkuu wa Mogadishu.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu tawi la Ujerumani itatoa msaada wa madawa na vifaa vya matibabu unaogharimu euro millioni moja.

Akizungumza mjini Berlin Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir alisema kuwa msaada huo, unaongeza orodha ya misaada ya kwa binaadam wanaokabiliwa na hali mbaya nchini Somalia, lakini akaonya kuwa hilo litawezekana iwapo machafuko yatamalizika.

Waziri Steinmeir amezitaka pande zinazohasimiana kuheshimu haki za binaadamu, kwa kuondoa vikwazo vinavyozuia misaada hiyo kuwafikia.

Kuanzia mwaka huu Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imetenga euro millioni 4 kwa ajili ya misaada ya kibinaadamu nchini Somalia.