1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani yalaani kuoneshwa hadharani rai wake wakiomba kuyanusuru maisha yao

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCl

Ujerumani imelaani kitendo cha kuoneshwa kwa mateka wawili raia wake, wakiomba kutekelezwa kwa matakwa ya wateji wao ili wasiuawe.

Watekaji nyara hao wamesema kuwa watawaua raia hao iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake huko Afghanistan ndani ya siku kumi.

Katika mkanda wa video uliyotolewa na watekaji hao, Hanerole Krause mwenye umri wa miaka 61 ameiomba serikali ya Ujerumani kutekeleza matakwa ya watekaji hao ili kunusuru maisha yake yake na mwanaye.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani amesema kuwa kamati inayoshughulikia mzozo wa mateka hao itakutana baadaye leo kujaribu kuutathmini mkanda huo wa video.

Krause akiwa na mwanaye wa kiume mwenye umri wa miaka 20 walitekwa nyara mjini Baghdad miezi miwili iliyopita.