1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Ujerumani kuwapa ruhusa ya kuishi wakimbizi.

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJK

Serikali ya mseto ya Ujerumani imefikia makubaliano ambayo yataruhusu mamia kwa maelfu ya watu kupata ruhusa ya kuishi nchini humo.

Wengi wa watu hao ni waliokuwa wakitafuta hifadhi ya kisiasa ambao maombi yao yalikataliwa, lakini waliruhusiwa kubaki nchini humo kwa misingi ya ubinadamu.

Chini ya makubaliano hayo, wale waliomo katika hali hiyo ambao wamekuwapo nchini Ujerumani kwa zaidi ya miaka sita, huenda wakapata ruhusa ya kuishi nchini humo moja kwa moja, ilimradi tu wapate kazi hadi ifikapo mwishoni mwa 2009.

Ruhusa yao ya hivi sasa ilikuwa ikiwanyima haki ya kupata kazi.