1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Rais wa Ujerumani ziarani, China na Vietnam

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0B

Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Horst Köhler anaanza ziara ya wiki moja katika nchi za Vietnam na China.

Shirika la kimataifa la haki za binaadam la Amnesty International tawi la Ujerumani, limemtaka Rais Köhler kuzungumzia suala la haki za binaadam atakapokuwa Beijing mji ambao ni mwenyeji wa michezo ya Olympic mwakani.

Kituo chake cha kwanza rais huyo wa Ujerumani kitakuwa Hanoi ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais Nguyen Mihn wa Vietnam juu ya elimu.

Kiasi cha waVietnam laki moja unusu wamesoma katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki ya kikoministi.