1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Rais Köhler kuamua iwapo atagombea wadhfa wake

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoY

Rais wa shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler hajaondoa uwezekano wa kupigania tena wadhfa wake ifikapo mwaka wa 2009.

Akihojiwa katika kipindi cha televisheni cha ARD – Sabine Christiansen rais Köhler amesema ataamua mwaka mmoja kabla ya muhula wake wa sasa kumalizika.

Rais Horst Köhler mnamo Julai mosi atakamilisha miaka mitatu tangu akabidhiwe wadhfa huo wa juu wa heshima nchini Ujerumani.

Wakati huo huo rais Köhler ametetea hoja ya rais wa shirikisho kuchaguliwa moja kwa moja na raia.