1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Rais Köhler akataa kumsamehe mpiganaji wa zamani wa Red Army

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC45

Rais Horst Köhler amekataa kutoa msamaha kwa mpiganaji wa zamani wa kundi la kigaidi la jeshi jekundu aliyekaa jela miaka 24.

Uamuzi huo umetolewa kwa waandishi wa habari kwa njia ya taarifa kutoka ofisi ya rais.Mpiganaji huyo wa zamani wa kundi la Jeshi jekundu Christiana Klar alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika visa vya mauaji vilivyoendeshwa na kundi hilo la kigaidi ikiwa ni pamoja na kuuwawa kwa mshtaki mkuu wa serikali Siegfried Buback kiasi miaka 30 iliyopita. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani awali ali

wataka watu waache kumshambulia rais Kohler baada ya wanachama wa ngazi ya juu wa chama chake cha kihafidhina kumkosoa vikali rais Köhler kwa kukutana na Christian Klar.

Baadhi ya wahafidhina walipendekeza bwana Kohler asichaguliwe tena kuwa rais akimaliza kipindi chake cha urais mwaka 2009 ikiwa atampa msamaha Christian Klar.