1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo akutana na rais Jacque Chirac wa Ufaransa

12 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3Z

Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel leo atakuwa na mazungumzo na rais Jaqcue Chirac mjini Paris nchini Ufaransa.

Mzozo wa ndege aina ya Airbus unatarajiwa kuwa mada muhimu katika mazungumzo baina ya viongozi hao.

Ujerumani na Ufaransa zinawakilisha sehemu muhimu katika kundi linalohusika na biashara ya safari za anga ambazo limekumbwa na mzozo wa kuchelewa kwa ndege za superjumbo A380.

Ubishi mkali kuhusu mageuzi umesasababisha mkuu wa kampuni hiyo ya Airbus bwana Christian Streiff kujiuzulu siku ya jumatatu baada kushindwa kuungwa mkono katika mapendekezo yake ya kupunguza wafanyakazi.

Rais mpya wa kampuni hiyo bwana Louis Gallois anatazamiwa kuzuru kiwanda cha Humburg leo hii amewaeleza wandishi wa habari kuwa hatua za kukifunga kiwanda hicho hazijamuliwa bado.