1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Fischer asema juhudi za kumkomboa Kurnaz kutoka Guantanamo zilishindwa

27 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOE

Waziri wa zamani wa mambo ya nje nchini Ujerumani Joschka Ficher amesema juhudi za iliyokuwa wizara yake za kumkomboa Murat Kurnaz kutoka jela ya Marekani ya Guantanamo zilishindwa.

Bwana Fischer akitoa ushahidi wake mbele ya kamati inayochunguza harakati za kupambana na ugaidi alisema wizara yake pamoja na mwenyewe binafsi walihusishwa katika kesi ya Kurnaz mzaliwa wa Ujerumani mwenye asili ya kituruki.

Amesema kwamba Marekani haikuwa tayari kumuachilia huru bwana Kurnaz.

Waziri wa sasa wa mambo ya nje nchini Ujerumani Frank-Waltersteinmeir ambaye wakati huo alikuwa mkuu anayehusika na haki na usawa anashutumiwa kwa kulikataa pendekezo la Marekani la kutaka kumuachilia Kurnaz mwaka 2002 kitendo ambacho kilisababisha hatimaye Kurnaz kuachiliwa mwezi Agosti mwaka jana 2006.