BERLIN:Chama kipya cha mlengo wa kushoto chaundwa Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 17.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Chama kipya cha mlengo wa kushoto chaundwa Ujerumani

Chama kipya cha mlengo wa kushoto kilichoundwa jana nchini Ujerumani kimeshutumiwa vikali na wanasiasa wa vyama vya kiliberali na SPD.

Mwenyekiti wa chama cha kiliberali bwana Westerwelle amesema kuwa chama hicho kipya ni tishio kwa Ujerumani.

Chama hicho kipya ni zao la muungano wa vyama viwili vya mlengo wa kushoto kutoka Ujerumani magharibi na mashariki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com