1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Bush aahidi kushirikiana na wenzake katika masuala ya mazingira

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBw0

Uingereza na Ujerumani zinaunga mkono kauli ya Rais wa Marekani George W Bush ya kushirikiana na wenzake wa kundi la G8 ili kuandaa mpango mpya wa kupunguza ongezeko la gesi za viwanda hewani.Rais Bush alieleza mipango yake ya kushirikiana na mataifa mengine tajiri ulimwenguni ili kuwa na lengo la kupunguza gesi za viwanda ulimwenguni.

Marekani iliyo mchafuzi mkubwa wa mazingira ulimwenguni haijatia saini makubaliano ya Kyoto ya kupunguza gesi za viwanda zinazosababisha ongezeko la joto ulimwenguni.

Bi Merkel aliye pia kiongozi wa kundi la G8 anasema kuwa mataifa yaliyostawi kiviwanda yanapaswa kutia juhudi zaidi kupunguza gesi za viwanda ulimwenguni.

Marekani kwa upande wake inasisitiza kuwa inakubaliana na kutafuta suluhu ya teknolojia wala sio kupunguziwa viwango vya gesi inazotoa jambo inalodai kuwa itaathiri ukuaji wa uchumi.