1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ziara rasmi ya kwanza ya Sarkozy

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1H

Rais mpya wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amekutana na Kansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel mjini Berlin,saa chache tu baada ya kiongozi huyo kuapishwa wadhifa wake mpya.Merkel alimshukuru Sarkozy kwa kufanya ziara yake rasmi ya kwanza ya kigeni kama rais,nchini Ujerumani.Viongozi hao wawili wamesema,watahakikisha kuwa Ufaransa na Ujerumani zitaendelea kuwa na ushirikiano wa karibu.Sarkozy pia alisisitiza dhima yake kufufua utaratibu uliozorota kuhusika na mfumo wa mageuzi katika Umoja wa Ulaya.Katiba mpya ya umoja huo imekwama tangu kupingwa katika kura ya maoni nchini Ufaransa na Uholanzi miaka miwili iliyopita.Hapo awali mjini Paris,Sarkozy katika hotuba yake ya kutawazwa alisema,atatimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi kuanzisha mageuzi makubwa yanayohitajiwa nchini humo katika sekta za uchumi na siasa.