1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ang'ang'ania mpango wake wa kutungua ndege zilizotekwa kwa hofu ya mashambulio ya kigaidi.

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdf

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble wa chama cha CDU amesema ataendeleza mpango wake wa kuruhusu ndege za abiria zilizotekwa nyara kuangushwa iwapo zitakuwa na uwezekano wa kusababisha mashambulio ya kigaidi.

Wolfgang Schäuble anashikilia msimamo wake huo ingawa suala hilo limezua mzozo kwenye muungano wa vyama unaotawala.

Msemaji wa serikali mjini Berlin amesema wizara zinazohusika zinachunguza pendekezo la serikali

Kulingana na pendekezo hilo, katiba ya Ujerumani inatakikana kubadilishwa hatua ambayo imewaudhi wanasiasa wa chama cha Social Democratic na vyama vingine vya upinzani.

Waziri Wolfgang Schäuble amesema hatari inayotókana na ndege iliyotekwa inapaswa kuchukuliwa kuwa na uwezekano wa kusababisha mashambulizi.

Bunge linahitaji thuluthi mbili ya wabunge kuidhinisha marekebisho ya katiba.