Berlin: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ziarani katika eneo la Milima ya Kaukas | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ziarani katika eneo la Milima ya Kaukas

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, leo anaanza kufanya ziara ya sikukadhaa katika eneo la Kusini mwa Milima ya Kaukas. Kwanza anatarajiwa katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, ambao atazungumzia juu ya maendeleo zaidi kuhusu siasa ya ujirani ya Umoja wa Ulaya. Azerbaijan ni nchi ya kuvutia kwa Ujerumani kutokana na utajiri wake wa mafuta na gesi ya ardhini, hasa ilivokuwa Ujerumani inatafuta uwezekano wa kupunguza kutegemea sana nishati ya kutokea Russia. Pia waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Ujerumani atazitembelea Georgia na Armenia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com