1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri asema kadhia ya Murat Kurnaz ilishughulikiwa kwa msingi wa kiusalama.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXD

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Otto Schily amemtetea Waziri wa Mambo ya nje, Frank-Walter Steinmeier kwa madai dhidi yake kwamba alikataa raia wa Ujerumani mwenye asili ya Kituruki kuachiwa huru kutoka gereza la Marekani la Guantanamo.

Murat Kurnaz hatimaye aliachiwa huru mwezi Agosti mwaka uliopita, miaka mitano baada ya kukamatwa nchini Pakistan kwa tuhuma za ugaidi.

Murat Kurnaz hakufunguliwa mashtaka yoyote.

Otto Schily alisema kadhia ya Murat Kurnaz ilihusu zaidi maswala ya usalama.