1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Watakaopinga mkutano wa G8 kukabiliwa vikali.

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC30

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble amesema anazingatia kuwaweka kizuizini watu wanaoshukiwa huenda watazusha ghasia kwenye mkutano wa mwezi ujao wa kundi la mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, utakaoandaliwa mjini Heiligendamm.

Waziri huyo amesema yamkini watu watawekwa korokoroni kwa kiasi wiki mbili iwapo kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba wana nia ya kuvuruga mkutano huo.

Maafisa wa serikali wanatarajia waandamanaji zaidi ya laki moja watajumuika katika eneo la mkutano huo kati ya tarehe sita na nane mwezi ujao.

Siku ya Jumatano iliyopita watu zaidi ya elfu tano waliandamana katika miji kadha ya Ujerumani wakipinga misako ya polisi iliyolenga maeneo arobaini yaliyohusishwa na wakereketwa wa mrengo wa kushoto.