1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wataalamu wanachunguza ujumbe katika video.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJl

Serikali ya Ujerumani imesema kuwa wataalamu wanafanya uchunguzi wa ujumbe katika kanda mbili za video zilizotumwa katika mtandao wa Internet, unaodhamiwa kuwa ni kutoka kwa mtandao wa magaidi.

Video ya hivi karibuni zaidi inatoa vitisho vya matumizi ya nguvu dhidi ya Ujerumani na Austria, iwapo nchi hizo hazitaondoa majeshi yao huko Afghanistan. Hii inafuatia video ya kwanza iliyotumwa siku ya Jumamosi ambapo wapiganaji wa Iraq wanaomshikilia mama mmoja wa Kijerumani pamoja na mwanae wa kiume wanatishia kumuua iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan katika muda wa siku kumi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schauble amesema kuwa kitisho hicho nchini Ujerumani kinazidi kukua.

Ujerumani ina wanajeshi 3,000 wanaotumikia jeshi la NATO nchini Afghanistan. Wawakilishi wa serikali ya Ujerumani wamesema kuwa nchi hiyo haipaswi kusalim amri kwa wapiganaji.