1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Wanasheria kumshtaki Rumsfeld

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsr

Kundi la wanasheria wa kimataifa linapanga kufunguwa kesi nchini Ujerumani dhidi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani anayeachilia ngazi Donald Rumsfeld na maafisa wengine kwa madai ya kuruhusu vitendo vya mateso.

Mawakili hao wanawawakilisha mahabusu wa zamani 11 wa Iraq wa gereza lenye sifa mbaya la Abu Ghraib lilioko karibu na Baghdad na mmojawapo wa mahabusu katika kituo cha mahabusu cha Guantanamo nchini Cuba.

Kesi hiyo inafunguliwa na wanasheria wa Marekani na Ujerumani chini ya sheria ya Ujerumani ambayo inaruhusu kuendeshwa kwa mashtaka ya uhalifu wa vita bila ya kujali mahali g ulikotendeka uhalifu huo.