BERLIN : Wahojiwa kwa kudhalilisha wafu | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Wahojiwa kwa kudhalilisha wafu

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imesema kwamba serikali inawahoji watuhumiwa 20 katika uchunguzi juu ya kudhalilishwa kwa mabufuru ya binaadamu kulikofanywa na wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Wanajeshi wawili walisimamishwa kazi wiki iliopita kwa kuhusika kwao katika tukio hilo baada ya gazeti la Bild la Ujerumani kuchapisha picha za wanajeshi wakiwa wamepiga picha na mabaki ya binaadamu.Msemaji wa wizara ya ulinzi amewaambia waandishi wa habari kwamba watuhumiwa hao 20 ambao hivi sasa wako chini ya uchunguzi ni wanajeshi wa vyeo vya chini,chini ya ngazi za uofisa.

Kansela Angela Merkel amekielezea kitendo hicho kuwa hakina msamaha na kwamba waliohusika wataadhibiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com