1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wabunge watakiwa kutozuwia kurefusha muda wa jeshi la kulinda amani Afghanistan.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBea

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amewaonya wanasiasa kutoruhusu hali ya hivi sasa ya utekaji nyara nchini Afghanistan kuwa na athari katika uamuzi wa kuongeza muda wa majeshi ya kulinda amani nchini huo.

Steinmeier ameliambia gazeti la Sächschen Zeitung, kuwa kikundi cha wizara ya mambo ya kigeni kinachoshughulikia masuala ya dharura kinafanyakazi kuweza kupata kuachiliwa kwa mhandisi wa Kijerumani ambaye alitekwa nyara wiki iliyopita.

Waziri huyo amesema matukio ya kusikitisha yaliyotokea hivi karibuni hayapaswi kuruhusu kugubika kile ambacho Ujerumani imefanikisha nchini Afghanistan katika muda wa miaka mitano katika ujenzi mpya wa kiuchumi.

Wajerumani wengi wanapinga kujiingiza kwa nchi hiyo katika ujumbe wa kulinda amani nchini Afghanistan na walishtushwa na kutekwa nyara kwa Wajerumani wawili, mmoja akiwa amekwisha kufa. Matokeo ya uchunguzi wa kidaktari yatatolewa wiki ijayo na maafisa wa Ujerumani.