1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Vyama katika serikali ya mseto watofautiana kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8q

Washirika katika serikali ya mseto ya Ujerumani wanatofautiana juu ya mapendekezo ya kupambana na ugaidi.

Wanachama wa chama cha Social Democratic wamesema kuwa hawataungamkono mpango huo uliopendekezwa na waziri wa mambo ya ndani kutoka chama cha Christian Democratic Wolfgang Schäuble.

Vyama hivyo viwili vinatofautiana juu ya pendekezo löa Schäuble la kutumia jeshi la ulinzi Bundeswehr kupambana na magaidi ndani ya nchi.

Wademocrat pia wanapinga kukubaliana na wazo lenye utata la kuwapa polisi uwezo wa kupata takwimu zilizohifadhiwa kielectroniki, kama vile hati za kusafiria pamoja na alama za vidole kwa raia wote wa Ujerumani.