Berlin. Ushahidi mpya wapatikana dhidi ya jeshi la Staasi. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Ushahidi mpya wapatikana dhidi ya jeshi la Staasi.

Nchini Ujerumani , waraka uliotangazwa mwishoni mwa juma umetoa ushahidi mpya wa amri ya maandishi kwa wanajeshi wa iliyokuwa Ujerumani ya mashariki DDR, kuwapiga risasi wale wanaotaka kutoroka kutoka nchini humo ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto , kwenda upande wa Ujerumani ya magharibi.

Waraka huo uliotolewa Oktoba mosi, 1973 na kupatikana wiki iliyopita katika ofisi ya nyaraka za zamani katika mji wa Magdenburg ulioko upande wa mashariki ya Ujerumani, unaonyesha kuwa wizara ya usalama wa taifa ambayo ilijulikana kama Staasi, iliwaamuru walinzi kuwa ni lazima wawazuwia ama kuwauwa, wale watakaojaribu kukimbilia upande wa magharibi.

Marianne Birthler, ambaye anaongoza idara inayoangalia ofisi hiyo ya askari kanzu wa Staasi, amesema waraka huo ni muhumu kwasababu viongozi wa kisiasa wa wakati huo wanaendelea kukana kuwa kulikuwa na amri hiyo ya kuuwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com