1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yaikosoa Burma kumzulilia nyumbani Aung San Suu Kyi

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByI

Ujerumani, ambayo inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, imetoa taarifa ya kukosoa uamuzi wa serikali ya Burma kuongeza muda wa kuzuiliwa nyumbani kiongozi wa upinzani, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi.

Kipindi cha mwaka mmoja cha agizo la sasa la kuzuiliwa nyumbani Aung San Suu Kyi kingekamilika kesho.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akizuiliwa nyumbani kwa zaidi ya miaka kumi na mmoja katika kipindi cha miaka kumi na saba iliyopita.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini Burma amesema hatua hiyo ni ya kinyama na haikubaliki.