1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani na kumbukumbu za wahanga wa vita vikuu vya dunia

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr3

Viongozi nchini Ujerumani jana waliongoza sherehe za kumbukumbu kuomboleza vifo vya watu waliouawa wakati wa vita. Sherehe zilifanyika katika jengo la makumbusho la mjini Berlin na kuongozwa na rais Horst Kohler na Kansela Angela Merkel. Baada ya hapo, viongozi hao wamewahotubia waarifiwa kwenye jengo la bunge. Bibi Merkel amesema kufundisha amani na maelewano ni msingi wa sera za Ujerumani wakzingatia watu waliofariki dunia katika vita vikuu viwili vya dunia. Hiyo inamaa kuchukuwa jukumu kubwa na kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi na machafuko ya kila aina.