1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani kupunguza matumizi ya umeme.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6q

Ujerumani inalenga kuimarisha matumizi yake ya nishati mbadala , wakati huo huo ikipunguza matumizi ya nishati na kuongeza matumizi ya mafuta yakibiolojia.

Akiwasilisha mpango wenye vipengee vinane ili kupambana na ujoto duniani katika bunge la Ujerumani, waziri wa mazingira Sigmar Gabriel amesema kuwa nchi hiyo inapaswa kupunguza matumizi ya umeme kwa asilimia 11 ifikapo mwaka 2020.

Amesema kuwa taifa hilo linapaswa kulenga katika kupata zaidi ya robo ya mahitaji yake ya nishati kutokana na jua, upepo na maji.

Gabriel amesema uimarishaji upatikanaji wa nishati salama kwa njia hii kutasaidia kupunguza utoaji wa gesi ya carbon kwa asilimia 40 ifikapo 2020.

Katika mkutano uliofanyika mwezi Juni mwaka jana wa kundi la mataifa nane yenye viwanda duniani nchini Ujerumani, kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliyataka mataifa , hususan Marekani , kuweka viwango maalum vya kupunguza gesi zinazochafua mazingira ambazo zinalaumiwa kwa kuleta ujoto duniani.