1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani kuongoza juhudi katika harakati ya kujikwamua kiuchumi.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe8

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema Ujerumani inapaswa kujitahidi mwaka huu wa 2007 ili kudumisha harakati zake za kujikwamua kiuchumi.

Kwenye hotuba yake ya mwaka mpya Angela Merkel alisema serikali yake itaendelea na mageuzi yake ya kijamii na ajira akisema kwamba maendeleo hayatapatikana bila matatizo kadha kuwepo.

Kuhusu maswala ya sera ya kigeni, Bi Merkel alisema serikali yake inalenga kusaidia kufufua mazungumzo yaliyokwama ya amani ya mashariki ya kati, na pia kushughulikia kwa kina suala la katiba ya Ulaya.

Kansela huyo alisema hakuna njia nyengine mwafaka kwa Bara la Ulaya kukabiliana na changamoto zinazotokana na utandawazi, ugaidi na vita, ila kwa kuungana.