1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani kujenga njia ya treni yendayo mbio nchini Iran.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwl

Kampuni la uhandisi la Ujerumani limesema kuwa limewasiliana na Iran juu ya ujenzi wa treni yendayo mbio. Msemaji wa kampuni hilo lenye makao yake makuu mjini Munich , Regierungsbaumeister Schlegel, amethibitisha ripoti iliyochapishwa katika gazeti la jana la Süddeutsche Zeitung, ambayo imesema kuwa Iran inataka huduma za kampuni hilo, zinazofahamika nchini Ujerumani kama Transrapid , ambapo itawachukua mahujaji milioni 12 hadi 15 kila mwaka kutoka Tehran hadi katika maeneo ya kidini nchini humo.

Baraza kuu la Wayahudi nchini Ujerumani limekosoa sana mpango huo, likisema kuwa wazo la kufanya biashara na Tehran ni kashfa kutokana na rais wa nchi hiyo Mahmoud Ahmedinejad kukana kuwa mauaji ya halaiki ya Holocaust hayakuwahi kutokea.