1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Tishio la mgomo wa madreva wa treni laitikisa Ujerumani

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmJ

Wasafiri wanaotumia usafiri wa treni nchini Ujerumani leo wameendelea kukabiliwa na tishio la mgomo wa madreva wa kampuni ya treni ya Ujerumani Deutsche Bahn.

Chama cha wafanyakazi kinachowawakilisha madreva hao, kimetishia kuitisha mgomo wa saa nne nchi nzima,kuchagiza ongezeko la asilimia 30 ya mshahara wanaodai madreva hao.

Vyama vingine viwili vya wafanyakazi pia vimetishia kuitisha mgomo huo, ambao utafanywa nyakati za asubuhi.