1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Steinmeier atakiwa kujieleza.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZL

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anaendelea kupata mbinyo kufuatia madai kuwa alizuia kuachiliwa huru kutoka katika jela ya Guantanamo Bay mfungwa Murat Kurnaz, mjerumani mwenye asili ya Kituruki.

Steinmeier alikuwa mkuu wa ofisi ya utawala katika ofisi ya kansela katika utawala ulipita.

Upande wa upinzani unataka maelezo kuhusu ni kwa nini serikali ya mseto iliyopita ya chama cha Social Democratic na Green ilishindwa kukubali ombi kutoka kwa serikali ya Marekani ya kumuachilia huru Kurnaz. Msemaji wa Steinmeier amesema kuwa waziri huyo atatoa taarifa katika tume ya uchunguzi ya bunge hivi karibuni.