1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Serikali yakataa madai ya kutuma ndege Afghanistan

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChQ

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imekataa madai ya vyombo vya habari kwamba serikali inapanga kutuma ndege za upepelezi za Tornado sita nchini Afghanistan pamoja na wanajeshi zaidi 250.

Hata hivyo naibu waziri wa ulinzi Gernot Erler amesema Ujerumani iko tayari kimsingi kupeleka ndege hizo kufuatia ombi la Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO lakini ameongeza kusema kwamba uamuzi huo bado haukutolewa.

Ujerumani hivi sasa ina wanajeshi 2,700 wanaotumika ndani ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF ambacho kinaongozwa na NATO nchini Afghanistan.

Serikali ya Ujerumani imekuwa ikikataa shinikizo la kuweka wanajeshi wake kusini mwa Aghanistan kusaidia vikosi vya NATO vilivyoemewa kupambana na uasi wa wanamgambo wa Taliban unaozidi kuongezeka.