1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Naibu kansela ajiuzulu.

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1b

Makamu wa kansela wa Ujerumani na waziri wa kazi , Franz Münterfering amejiuzulu. Alikuwa kiongozi mwandamizi katika chama cha Social Democrats katika muungano unaounda serikali na chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union CDU. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 67 amesisitiza kuwa uamuzi wake ni wa binafsi na hauna sababu za kisiasa. Mke wa Müntefering amekuwa akiugua saratani, yaani kansa kwa miaka kadha na kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Müntefering amesema kuwa atakayechukua nafasi yake kama makamu kansela ni waziri wa mambo ya kigeni Frank-Walter Steinmeier.