1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mwito kurefusha ujumbe nchini Afghanistan

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQL

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ametoa mwito kwa bunge,kuunga mkono mpango unaopendekeza kurefusha ujumbe wa Ujerumani unaolinda amani nchini Afghanistan.Wakati wa mdahalo wa bajeti ya mwaka 2008,Merkel alisema,majeshi ya Ujerumani yanapaswa kubakia nchini Afghanistan mpaka vikosi vya nchi hiyo vitakapoweza kuhakikisha usalama. Chama cha upinzani cha FDP,kimetumia mdahalo wa bajeti kuikosoa serikali ya mseto ya Merkel kuwa raia wa kawaida wa Ujerumani hawanufaiki na uchumi ulioinuka hivi sasa nchini humu.Merkel amepuza lawama hizo na kusema,idadi ya wakosa ajira imepunguka tangu serikali yake ya mseto kushika madaraka miaka miwili iliyopita.