1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mwenyekiti ya bodi ya kampuni la Siemens kujiuzulu.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8r

Mwenyekiti mwangalizi wa bodi ya kampuni kubwa la vifaa vya electroniki nchini Ujerumani la Siemens amesema kuwa atajiuzulu kutoka wadhifa wake.

Taarifa ya kampuni hilo imesema kuwa Heinrich von Pierer atajiuzulu wakati wa mkutano ujao wa bodi hiyo hapo Aprili 25.

Von Pierer, hata hivyo , amekana kuhusika binafsi katika kashfa ya hivi karibuni, ikiwa ni tuhuma za fedha za hongo iliyotumika kupata mikataba nchi za nje.

Mbinyo umeongezeka katika wiki za hivi karibuni kwa Von Pierer, ambaye alikuwa mkuu wa Siemens katika miaka ambapo utaratibu wa kutenga fedha za hongo ulianzishwa.

Amesema kuwa anajiuzulu kwa manufaa ya maslahi ya kampuni hiyo.