1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkutano wa Mfuko wa Dunia wafunguliwa

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMF

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan leo amefunguwa mjini Berlin kile alichokieleza kuwa juhudi moja kubwa kabisa ya kugharamia afya duniani ambayo haikuwahi kufanyika kabla katika mkutano wa wafadhili kwa ajili ya Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI,kifua kiuu na malaria.

Annan amesema lengo ni kuwa na mchango wa fedha wa dola bilioni sita ifikapo mwaka 2010 na hatimae kuziongeza fedha hizo hadi kufikia bilioni nane.

Kwa mujibu wa Annan mfuko huo ambao umeanzishwa mapema mwaka 2002 kufuatia uamuzi wa Kundi la Mataifa Manane Tajiri Duniani huko Genoa mwaka mmoja kabla tayari umeidhinisha matumizi ya dola bilioni nane nukta nne.

Mfuko huo umetowa msaada kwa wagonjwa milioni moja nukta moja wa UKIMWI na wagonjwa milioni 3.3 wa kifua kikuu pamoja na mamilioni ya vyandaruwa vya kujikinga na mbu.