1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mjadala mkali wazuka kuhusu uhamiaji.

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBj0

Mjadala mkali kuhusiana na uhamiaji umezuka katika serikali ya mseto nchini Ujerumani, siku moja baada ya mkutano baina ya serikali na viongozi wa makundi ya kijamii mjini Berlin.

Mtaalamu wa masuala ya mambo ya ndani katika chama cha Social Democratic ameelezea ukosoaji wake kwa mkutano huo akisema kuwa muda umefika kwa wahamiaji walioishi katika nchi hii kwa muda mrefu kupewa haki ya kupiga kura katika chaguzi za majimbo.

Msemaji wa chama cha kansela Angela Merkel Christian Democratic amepuuza mawazo hayo, akisema kuwa hali hiyo haitoi nafasi ya motisha kwa utoaji wa uraia.

Siku ya Alhamis , Merkel aliueleza kuwa ni alama muhimu mpango mpya wa ujumuisho wa kitaifa kwa ajili ya wahamiaji nchini humo, licha ya ususiaji wa makundi matatu makubwa ya jamii ya Waturuki katika mkutano huo.

Makundi hayo yalikuwa yanapinga dhidi ya sheria za hivi karibuni ambazo zinaweka vikwazo kwa wahamiaji kuleta familia zao nchini humo.