1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel atumai amani Mashariki ya Kati

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXI
Rais Bush na waziri mkuu wa Australia Howard
Rais Bush na waziri mkuu wa Australia HowardPicha: AP

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameonya juu ya tishio kubwa kwa Mashariki ya Kati iwapo mazungunmzo kati ya Israel na Wapalestina hayatoendelezwa.

Akizungumza baada ya kukutana na Mfalme Abdallah wa Jordan mjini Berlin Kansela huyo wa Ujerumani amesema anaona kuna mwanga wa matumaini kwa kupiga hatua katika mchakato wa amani Mashariki ya Kati.Mazungumzo yao yanakuja ikiwa ni wiki moja kabla ya Merkel kuanza ziara ya Mashariki ya Kati ambapo atakutana na viongozi wa Misri,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait.

Wakati huo huo kundi la pande nne linaloshughulikia amani ya Mashariki ya Kati ambalo linajumuisha Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa,Urusi na Marekani linatazamiwa kukutana mjini Washington Ijumaa ijayo.