1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel anahimiza kupunguza ongezeko la joto duniani

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRc

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema,kipindi cha Ujerumani kama rais wa Umoja wa Ulaya kitumiwe kuisaidia Ulaya kushika nafasi ya mbele kupunguza gesi zinazochafua mazingira.Hata hivyo, amesema,Ulaya peke yake,haiwezi kutenzua tatizo hilo kwani asilimia 15 tu ya gesi zinazochafua mazingira,husababishwa na Ulaya.Akizungumza mbele ya baraza la wawakilishi wa serikali za majimbo-Bundesrat-Kansela Merkel aliongezea kuwa Umoja wa Ulaya lazima utafute njia za kuziingiza Marekani na nchi zinazoinukia kiuchumi,katika makubaliano ya kimataifa.Akaongezea kwamba Ujerumani inaunga mkono mapendekezo ya Umoja wa Ulaya kuwa hadi mwaka 2020,asilimia 20 ya nishati katika nchi hizo ipatikane kwa njia za mbadala ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.