1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN :Kansela Angela Merkel kuzuru Uchina na Japan wiki hii

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVk

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ameanza ziara yake ya siku sita nchini Uchina na Japan inayolenga kutia nguvu juhudi zake za kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya anga.Bi Merkel anatarajiwa kutoa hutuba nchini Japan kuadhimisha miaka 10 tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya Kyoto ya kupambana na athari za hali ya anga vilevile kushawishi nchi ya Uchina kutia juhudi zaidi kupunguza kiwango chake cha gesi za viwanda.

Bi Merkel anafanya ziara hii kama kiongozi wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda G8.

Mazungumzo ya viongozi hao yanatarajiwa kugusia juhudi za kidiplomasia ili kutafuta suluhu katika mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini na Iran aidha suala la ghasia nchini Afghanistan.

Bi Merkel anaandamana na ujumbe wa wafanyibiashara 25 kutoka eneo la Asia na Pacific na kutarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Uchina Hu Jinatao ,Waziri Mkuu Wen Jiabao aidha makundi ya kisheria na kitamaduni nchini Uchina.

Japan inachukua uongozi wa kundi la mataifa 8 yaliyostawi kiviwanda G8 mwaka ujao na ziara ya Bi Merkel inapanga kuipa msukumo hatua hiyo.Kansela Angela Merkel atakutana na Emepror Akihito pamoja na Waziri Mkuu Shinzo Abe.

Hii ni ziara yake ya pili nchini Uchina kama kansela wa Ujerumani nay a kwanza nchini Japan atakakowasili siku ya jumatano.Pia atahudhuria michezo ya olimpiki ya Ulimwengu mjini Osaka.