1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Atishiwa maisha kwa kushutumu vazi la hijabu

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCxG

Viongozi wa makundi ya Waislamu nchini Ujerumani na chama cha Kijani wameelezea kujizatiti kwao kwa uhuru wa kutowa maoni na kulaani vitisho vya kifo dhidi ya mbunge wa chama cha Kijani Ekin Deligoz.

Deligoz ambaye alitowa wito kwa wanawake wa Kiislam kuvuwa hijabu vitambaa wanavyojifunika kichwani amekuwa akipatiwa ulinzi wa polisi.Mbunge huyo wa kike pia amekuwa akiungwa mkono kwa hali na vyama vya kihafidhina nchini Ujerumani vya CDU na CSU.

Msimamo wa mwanamke huyo juu ya hijabu umeshutumiwa na msemaji wa Waislamu.

Ujerumani ina takriban Waislamu milioni 3 wengi wao wakiwa ni wa asili ya Uturuki.