BERLIN: Abbas akutana na Merkel | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Abbas akutana na Merkel

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas anakutana na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel mjini Berlin hapa Ujerumani.

Baada ya kukutana hapo awali na waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, rais Abbas ametoa mwito mgomo dhidi ya serikali ya Palestina kufuatia ushindi wa kundi la Hamas kwenye uchaguzi wa bunge, umalizike.

Waziri Steinmeier alisisitiza sharti la pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya Mashariki ya Kati kwamba serikali mpya ya Palestina itatakikwa ilaani machafuko na iitambue haki ya kuwepo kwa taifa la Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com